Wizara ya Afya chini ya uongozi wa Dr. Juma Duni (pichani) imetokeza ghafla kuwa yenye maendeleo makubwa.Licha ya kuwa wagonjwa na watu wanaolazimika kukaa nao hapo hospitali wanapewa kwa dasturi chakula mara tatu kila siku na kupewa matunda, kama vile machungwa, ndizi; kuna mengi ya maendeleo.
Ule mtindo wa wagonjwa wawili kulazwa kitanda kimoja, au hata kulala chini; umeondoshwa. Kumbukumbu za wagonjwa zote au nyingi zimeshatiwa kwenye komputa, na kila mgonjwa kupewa kadi yake ya hospitali, hivyo imeondowa ule mtindo wa mgonjwa kwenda hospitali na buku la kumbukumbu zake.
Dawa zinatolewa kwa cheti cha dawa cha desturi, si kama vile ilivyokuwa - kwa karatasi tu. Takriban dawa zote zinapatikana hospitali bila ya malipo au taabu yoyote.
Unadhifu pia unatia furaha, hospitali inanukia harufu nzuri ya kihospitali, madaktari na wauguzaji wanang'ara na kuonesha furaha nyusoni mwao. Lifti zinafanyakazi kwa uhakika.
Yote haya, japokuwa ni juhudi za Dr. Juma Duni; lakini ni kwa kushirikiana kikamilifu wafanyakazi wote wa wizara ya Afya. Inshaallah na wizara mengine, khasa Wizara ya Elimu, Wizara ya Elimu ya juu na Wizara ya Fedha, zitatokeza juu kuonesha maendeleo yao.
Tunatakia ziada ya maendeleo kwa jumla.


Toa Maoni Yako:
0 comments: