Mara baada ya kumaliza kupokea adhabu ya viboko mama huyu alipoteza fahamu na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Watu waliohudhuria adhabu ya mama huyo wakimbeba kumkimbiza hospitali baada ya kupoteza fahamu.

---

Gazeti la Jakarta Globe linaripoti kwamba mwanamke mmoja raia wa Indonesia amechapwa bakora mbele ya msikiti baada ya kukutwa na hatia ya kufanya tendo la ndoa katika kipindi ambacho alikuwa katika harakati za kuhitimisha talaka yake toka kwa mumewe wa awali.

Irdyanti Mukhtar, 34, alitandikwa bakora tisa kwa kosa la uzinzi mbele ya kadamnasi ya watu 200 waliokuwa wakishangilia kwa nguvu nje ya msikiti wa Al Munawwarah, katika mji wa Jantho.

Mukhtar alihukumiwa siku moja kabla na mahakama ya Kiislamu inayoendesha shughuli zake kwa msingi wa Sharia. Mwendesha mashtaka alisema Mukhtar alikutwa akiwa na mahusiano ya karibu na mwanaume mwingine angali bado kukamilisha talaka yake kwa mumewe wa awali.

Gazeti hilo linaendelea kuripoti kwamba mama huyu alikuwa ni mmoja kati ya watu wanne, akiwemo mwanaume anayesemekana kuzini nae, kutumikia adhabu hiyo ya viboko.

Polisi ambao pia wanafanya kazi chini ya mfumo wa Sharia wanafanya uchunguzi juu ya tuhuma za mama huyu kwamba alidhalilishwa na kadamnasi kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mara baada ya kumaliza kupokea adhabu hiyo ya viboko mama huyu alipoteza fahamu na alikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: