Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge leo kuhusu sababu za vurugu na uahirishaji wa zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa katiba mpya kwa mikoa ya Dodoma , Dar es salaam na upande wa Zanzibar ambako zoezi linafanyika leo.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akijibu maswali ya wabunge yaliyoulizwa kuhusu vyombo vya studio vya kurekodia walivyopewa wasanii na Rais Jakaya Kikwete ili kupunguza matatizo wanayoyapata katika kazi zao ambapo amesema utaratibu wa ufungaji wa studio hiyo unafanyika ili kutoa fursa kwa wasanii wengi kunufaika kwa gharama nafuu.
Baadhi ya maofisa wa JWTZ na watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa wakitoa salam kwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kutambua uwepo wao ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Raia wa kigeni wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma ambako walipata fursa ya kufuatilia mijadala ya wabunge.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku (kushoto) akizungumza jambo na Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu waziri wa Ujenzi Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi (katikati) na Mh. Zakia Meghji (Mbunge wa viti maalum, CCM) nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kufuatia vurugu zilizotokea jana wakati wa zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa katiba mpya ambapo ametoa wito kwa serikali kuongeza muda zaidi wa ukusanyaji wa maoni na idadi ya mikoa ambayo itashiriki katika zoezi hilo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda (katikati) akizungumza na Bw. Anic Kashasha (wa pili kutoka kushoto) mtendaji mkuu wa kampuni ya Tricy Solutions ya jijini Dar es salaam inayojihusisha na utoaji wa huduma na biashara ya vifaa vya umwagiliaji wa dawa za kuulia wadudu, Bajaj au Pikipiki maalum za kubebea wagonjwa na vifaa vya kuzimia moto leo katika viwanja vya Bunge Dodoma.
Mbunge wa Longido Mh. Michael Lekule Laizer akitelemka ndani ya pikipiki maalum ya kubebea wagonjwa aliyopewa na Waziri mkuu Mizengo Pinda kusaidia wananchi wa jimbo lake leo mjini Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: