Bondia mtanzania Deo Njiku ameondoka nchini hii leo kuelekea Ufilipino kwa ajili ya pambano la ubingwa wa Dunia uzito mwepesi dhidi ya bondia wa huko Pank Gonzayael.

Wakiongea kabla ya kupanda ndege kuelekea Ufilipino, mratibu wa pambano hilo kutoka kamisheni ya masumbwi nchini, Antony Lutta amesema huo ni mwendelezo wa kuwatangaza mabondia wa Tanzania nje ya nchi huku bondia Deo Njiku akiwa na imani ya kufanya vema na hatimaye kupata mkanda wa kwanza wa Dunia.

Bondia Njiku anayetoka mkoa wa Morogoro katika kambi ya bondia maarufu nchini Fransis Cheka atapanda ulingoni kuumana na Gonzayael anayetoka kambi ya bingwa wa Dunia, Manny Pacquiao.

Pambano hilo litakalofanyika Aprili 9 mwaka huu jijini Manila ni la kwanza la kimataifa kwa Deo Njiku ambaye amepigana mapambano kumi na sita hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: