Wafanyakazi wa Zain Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahabusu ya watoto wadogo ya Upanga jijini Dar es Salaam waliopotembelea jana.
Mwalimu Margaret Lubeleje (kulia) anayefundisha watoto katika Mahabusu ya watoto wadogo ya Upanga jijini Dar es Salaam akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania Tunu Kavishe (kushoto). Kampuni ya Zain jana ilitoa msaada wa vitabu mbalimbali katika mahabusu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania Tunu Kavishe (kushoto) akitoa shukrani zake kwa uongozi wa mahabusu hiyo.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania Tunu Kavishe (kulia) akizungumza na watoto ambao ni mahabusu wa kituo hicho kabla hawajatoa msaada.
Afisa Maendeleo ya jamii Wolfgang Kimaro akiongoza wageni kutoka Zain Tanzania waliotembelea mahabusu hiyo kuelekea ndani ya mahabusu.
Afisa Maendeleo ya jamii Wolfgang Kimaro pamoja na Mwalimu Margaret Lubeleje wakizungumza na wafanyakazi wa Zain Tanzania walioambatana katika kutoa msaada huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: