Picha hii tumeipata katika mtandao wa BBC. Kama ulivyosikia, misaada imeanza kuwasili, watu wanachanga fedha na mali, pia wanajitolea kwa kila hali ikiwemo kwenda Haiti kufanya shughuli za kujitolea kama si kuandaa maonesho ya muziki ili kuchangisha fedha za kufanikisha uokoaji wa watu toka kwenye janga la Haiti, lilisobabishwa na tetemeko kubwa kabisa la ardhi.

Lakini ukweli ni kwamba tumeelekeza macho yetu kwa Haiti kama Taifa, tumesahau shida zinazowakumba Wa-Haiti kama mtu mmojammoja. Katika picha hii unaweza kuona mama huyu akinyang'anywa bidhaa zake za msaada alizopatiwa na wasamaria wema. Wanaomnyang'anya huwezi kuwaita wezi, ni waathirika wenzake. Ukweli ni kwamba hali ya usalama katika Haiti, ukiacha janga la tetemeko, ni mtihani mkubwa kwa serikali ya Haiti, na wananchi hawako salama sana. Hali inapofikia namna hii hatuna budi, japo kwa sekunde 10 kila siku, kusema "Muumba elekeza macho yako kwa watu wa Haiti, Amen."

Picha na AFP
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: