Mwenyekiti wa Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la Kusini, Mchungaji Clement Mwaitembele alisema zinahitajika juhudi za pamoja katika kuwajengea uwezo wanawake hususani waishio vijijini ili wawe na uwezo wa kujitegemea badala ya kutegemmea kwa waume zao kwa kila kitu.

Akizungumza na wanawake zaidi ya 30 ammbao wanahudhuria mmafunzo ya kupambana na umaskini vijijini wanakoishi Mchungaji Mwaitembele, alisema wanawake wengi wamekuwa na mazoea ya kuwategemmea wanaume zao katika kuendesha aisha yao ya kifamnilia jambo ambalo umekuwa mzigo na kuwa chanzo cha unyanyasaji kwani mwanaume anakuwa na ubabe wa kimaamuzi mwanamke kukosa haki ndani ya nyumba.

Alisema juhudi hizo zinahitajika kwa mmashirika ya kidini na kiraiya kuwasaidia wanawake
nchioni ambao wamekosa sauti ya pamoja ambayo inaweza kusikika wakakombolewa,pamoja na
juhudi zilizofanyika za kuwepo kwa wanawake ambao ni viongozi katika serikali lakini wanawake wanaoishi vijijini hawajafunguliwa kiufahamu kutambua kwamba wanaweza bila ya waume zao.

Mafunzo haya ya kuwajengea uwezo wanawake yameanza leo wilayani Kyela ambayo yaedhaminiwa na shirika la misaada ya NORWEGIAN CHURCH AID-NCA, ambapo yataendelea katika wilaya zote za mkoa wa mbeya hasa vijijini, kwani huko kuna wanawake wengi ambao hawajajua elimu ya kujikwamua kiuchumi na kupambana na umaskini.

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo kutoka NCA Mchungaji Blandina Sawayael alisema wanawake wanaweza wakiwezeshwa,lakini hakuna mitandao ambayo imefika vijijini itakayoweza kusikia sauti za wanawake na kutambua shida zinazowakabili huko vijijini,bali mitandao inayoanzishwa ya kushughulikia matatizo ya wanawake inaishia maeneo ya mijini.

Mchungaji Sawayael alisema ni wakati sasa mmashirika yote yaliyo na usajili wa kudumu
yanayoshughulika na wanawake waelekeze mipango yao vijijini kwani mambo engi akinamama
waishio vijijini wanaogopa kusema ili wasaidiwe.

NCA ni shirika ambalo limekuwa likitoa elimu kwa akina mmamma ili wapate uwezo wa
kujitegemea kwa kujishughulisha na miradi yoyote kwa lengo la kuacha kutegemea kila kitu kwa
waume zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: