Kushindwa kwa ushawishi wa kisiasa pamoja na kidini kumetajwa kuwa kunachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vitendo vya rushwa hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi,ofisi ya Makamu wa Rais–Utawala Bora wakati akiungumza na wafanyakazi wa Sekretarieti ya maadiliya viongozi wa umma mjini DODOMA. Mheshimiwa SOPHIA SIMBA (pichani) amesema mmomonyoko wa maadili usiojali walakuogopa maadili ya kazi ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la rushwa hapanchini.
Ameeleza mafanikio dhidi ya rushwa yatategemea kwa kiasi kikubwaushirikiano wa nguvu za dola na kisheria , jamii, dhamira ya kisiasa namaadili binafsi katika kukomesha tatizo hilo haspa nchini.

Mheshimiwa SIMBA amezungumza na wafanyakazi hao wakati wa kufungua mkutano wa sita wa baraza la wafanyakazi na semina ya siku moja kuhusurushwa na huduma kwa wateja inayofanyika mjini DODOMA .

Mapema kamishina wa maadili na mwenyekiti wa baraza hilo lawafanyakazi mheshimniwa Jaji STEPHEN IHEMA amesema kuwa sekretarieti hiyoinatambua kilio kikubwa cha wananchi kuhusiana na rushwa ambapo imewekamikakati ya kupambana na tatizo hilo ndani na nje ya nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: