Jeshi la Polisi Mkoani RUVUMA linamshikilia Mkazi mmoja wa kijiji cha LITOLA katika wilaya ya NAMTUMBO baada ya kukamatwa akiishi kinyumba na mwanafunzi wa darasa la tano.
Kamanda wa Polisi Mkoani RUVUMA Bwana FALHUM MSHANA amesema mtuhumiwa huyo SAID KANDURU mwenye umri wa miaka 38 amekamatwa tangu tarehe 31 mwezi uliopita akiwa amelala nyumbani kwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 13.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunafuatia juhudi zilizofanywa na Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha LITOLA Bwana MAXIMILIAN KOMBA aliyeweka mtego na kumnasa usiku wa manane akitumia askari mgambo na wananchi.
Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo alikuwa na mawasiliano na bibi wa Binti huyo, kwa makubaliano ya kumwozesha.
Mkoa wa RUVUMA ni kati ya mikoa inayokabiliwa na tatizo la idadi kubwa ya watoto wa shule kukatisha masomo kwa kupata ujauzito, kunakotokana na tabia za baadhi ya wanaume kufanya mapenzi na watoto wa shule.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: