Moto mkubwa unaodaiwa kuwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme umesababaisha hasara ya mamilioni ya pesa baada ya kuteketeza sehemu kubwa ya hoteli ya kitalii ya Protea iliyopo katika eneo la Oysterbay Jijini. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amesema tukio hilo limetokea mishale ya saa 7:00, usiku wa kuamkia jana. Amesema moto huo uliteketeza sehemu ya jiko ya hoteli hiyo inayomilikiwa na Rahim Gangiji, 31 na kisha kuteketeza mali yote iliyokuwamo. Amesema moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa wananchi, Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Jiji na Kampuni binafsi ya Ultimate Security.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: