Bishanga alikumbwa na mkasa huo usiku wa kuamkia Aprili 14, mwaka huu nyumbani kwake Makumbusho, jijini Dar es Salaam baada ya jiko la gesi wanalotumia kumlipukia saa 7. 20 usiku.
Kufuatia mlipuko huo, Bishanga aliungua vibaya sehemu mbali mbali za mwili na kupoteza fahamu, hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam akiwa hoi bin taaban.
Mwandishi wetu alifanikiwa kufika katika hospitali hiyo na kumkuta Bishanga akiwa amelazwa katika ghorofa ya 2 wodi namba 2 huku mkewe akiwa pembeni yake akimuuguza.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa tabu, msanii huyo alisema kuwa, siku ya tukio alikuwa amelala na mkewe, Terry Godfrey aliyemuoa hivi karibuni na ilipotimu saa 7.20 usiku, alisikia harufu ya gesi ikiwa imetapakaa chumba kizima.
Kufuatia harufu hiyo, Bishanga alisema kuwa alilazimika kwenda jikoni kulikokuwa na jiko la gesi kuangalia kilichotokea, lakini alipofungua mlango tu, mlipuko mkubwa wa gesi ulitokea na kusababisha aungue mwilini.
“Nikiwa nimelala nilishtuka usingizini baada ya hewa kuwa nzito na nilipoamka nilibaini harufu iliyotanda chumbani ilikuwa ni ya gesi hivyo, nikaamua kwenda jikoni kutazama mtungi wake kama ulikuwa una tatizo lakini nilipofungua nilikaribishwa na mlipuko ulioniunguza mwilini kama unavyoniona,” alisema Bishanga.
Kwa upande wake mke wa msanii huyo, Terry alisema kuwa, alishtuka usingizini baada ya kusikia kelele za mumewe aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuungua ambapo baba mwenye nyumba naye alisikia kelele hizo hivyo kuungana pamoja na majirani kisha kumkimbiza msanii huyo hospitali. “Mume wangu kipenzi ameungua sana! Sijui ni mkosi gani huu kwani ndoa yetu bado changa, hatujamaliza hata mwaka nakumbana na majaribu makubwa kama haya,” alisema Terry.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: