TIGO wadhamini wa ziara ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Hip Hop toka nchini Marekani, Curtis Jackson maarufu kama ‘50 Cent’ wameweka wazi kuwa sasa wapo kamili kabisa na wataanza kuuza tiketi za kumuona mwanamuziki huyo kuanzia wiki ijayo.

Meneja Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo , Kelvin Twissa ambao ndio wadhamini wakuu wakishirikiana na kampuni ya prime time promotions wanaomleta mwanamuziki huyo hapa nchini,amesema kuwa watauza tiketi chache kukwepa watu kujazana katika onyesho.

“ Tiketi za onyesho la 50 Cent zitaanza kuuzwa Jumatatu ijayo na tutakuwa na tiketi chache ili kuepuka watu kujazana sana kwenye shoo hiyo, hivyo kwa wale mashabiki wa muziki wanaombwa kuwahi kununua tiketi zao ili kuepuka usumbufu” alisema Twissa.

Tiketi za kushuhudia onyesho hilo la 50 Cent zitauzwa kwa Sh 50,000 kwa wale watakaokaa viti maalum, na 30,000 kwa wale watakaokaa sehemu ya kawaida na kuwahi kununua tiketi zao mapema lakini wale watakaochelewa kununua na kununulia mlangonitiketi zao, siku ya onyesho watalipa Sh 40,000.

Onyesho la 50 Cent pamoja na wenzake wa kundi la G-Unit linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa muziki wa Hip Hop hapa nchini limepangwa Kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Mei 4,2008.

Wakati huohuo jana Tigo iliendesha droo ya kwanza ya promosheni kwa wateja wake kwa lengo la kutoa tiketi 200 za kwanza kati ya tiketi 700 zitakazotolewa na Tigo kwa wateja wake ili kushuhudia onyesho la mwanamuziki 50 Cent.Katika droo ya pili ambayo itafanyika wiki ijayo watapatikana washindi 300 na ya mwishoni 200 ili kutimiza washindi 700, watakaoshuhudia onyesho hilo.

Kushiriki katika promosheni hiyo unatakiwa kutuma neno muziki ama ‘Music’ kwenda namba 15315 nabaada ya hapo uatingizwa kwenye droo ya kupata washindi.

Mwanamuziki 50 Cent anayetoka katika jiji la New York nchini Marekani anatamba albamu za ‘Get Rich or Die Tryin’ na ‘Massacre' ambazo zilimpatia tuzo mbalimbali huko Marekani aikiwa na nyimbo kama ‘In da Club’ , ‘I get money’ , Straightto the bank’ na Amusement Park .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: