Ni vigumu kuamini lakini hakika ndivyo ilivyo. Wahenga walisema ukistajabu ya Mussa basi utaona ya firauni! Hakika mapenzi yanatesa.
Ni mkasa wa kusikitisha ulimkuta kijana ambaye kutokana na matatizo hayo ameona ni bora picha zake ziaktumika kueleza jamii ya Watanzania namna anavyoteseka na chanzo cha mateso hayo kikiwa ni mapenzi na kwake sasa yametumbukia nyongo na anaiona dunia ni chungu.
"Ama kweli hujafa hujaumbika, leo nimekuwa mtu wa kushindwa kutembea, lakini kinachoniuma zaidi ni kushindwa kufanya tendo la ndoa, siwezi kufanya mapenzi kutokana na hali niliyonayo sasa."Bora matende haya ya ajabu yangenitokea katika mguu, lakini hili jingine ambalo limenitokea sehemu ya ndoa, kwa kweli nateseka, nashindwa kuelewa mtu unalala mzima asubuhi unaamka na matende!
"Nina imani aliyenifanyia hivi ni sababu ya wivu wa kimapenzi, ni mapenzi, ni wivu...ni wivu wa kimapenzi tu ndio umenifanya leo hii niwe katika hali hii, inasikitisha sana, naomba Watanzania wenzangu wanisaidie," ndivyo Musa Paulo anavyoanza kueleza mkasa wa aina yake uliomkuta.
Paulo ni mkazi wa wilaya ya Bariadi mkoa wa Shinyanga mwenye miaka 23, ameugua ugonjwa wa ajabu na kumfanya aishi kwa shida na mateso makubwa baada ya kuachana na mpenzi wake kitu anachoamini kuwa chanzo ya ugonjwa huo alioupata ghafla.
Akizungumza,Paulo anasema chanzo cha ugonjwa huo ambao amedumu nao kwa miaka mitatu sasa hakijajulikana hasa kwa mujibu wa uchunguzi wa hospitali. Amevimba mguu wa kulia kama tende kuanzia kwenye nyayo hadi katika paja, lakini zaidi amevimba sehemu za siri tende kubwa kama tunda la fenesi.
Anasema ugonjwa huo alimpata siku moja tu kwa ghafla. Siku hiyo alihisi baridi mwili na kisha ganzi katika mguu wa kulia na sirini . Alitoka kula jioni hiyo na rafiki zake kwenye mgahawa mmoja. Alfajiri yake aliamka na kukuta mguu umevimba hadi sehemu za siri huku misuli ya mguu imekaza mno ikiambatana na maumivu makali kiasi na kushinwa kunyanyuka kitandani.
"Ninahisi baada ya kuachana na mpenzi wangu, ndiye aliyenifanya hivi kwa sababu alikuwa na wivu sana na hakupenda nimwache na mara kwa mara alikuwa kinitisha kwamba siku nitakayomwacha nitakiona cha moto," anaeleza Paulo na kuongezea;
Wadau kwa mujibu wa Bw Musa Paulo ni kwamba Daktari aliyempokea alimueleza kuwa tatizo lake linaweza kwisha kwa kufanyiwa upasuaji unaogharimu shilingi laki sita,lakini hana uwezo wa kupata pesa hizo,kutokana na kuteseka sana anawaomba wasamaria wema na watanzania kwa ujumla popote walipo watakaoguswa na ugonjwa huu wamsaidie," Kwa wale watakaopenda kumsaidia Bw. Musa Paulo mnaweza kuwasiliana nae kupitia simu number (0732-094755)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: