Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na wadau wa michezo ya watu wenye ulemavu, tunatoa pongezi za dhati kwa MR. TUMA DANDI kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC).

Tunatambua mchango mkubwa wa International Paralympic Committee pamoja na vyama vyote vinavyosimamiwa na TPC, wadau wa michezo, na mamlaka mbalimbali zinazosimamia maendeleo ya michezo nchini kwa kuendelea kuunga mkono ushirikishwaji, maendeleo na mafanikio ya wanamichezo wenye ulemavu.

Tunaamini uongozi wako utaendelea kuimarisha mshikamano, maendeleo ya michezo ya Paralympic na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: