Makamu wa Rais aliongeza kuwa katika uongozi wake, hayati Magufuli alionesha ujasiri na uthubutu mkubwa katika kufanya maamuzi magumu yenye maslahi kwa taifa, huku akisimamia kwa dhati misingi ya haki na usawa kwa wananchi wote.
Aidha, alisema hayati Magufuli hakusita kupambana na vitendo vya uzembe na rushwa, na alihimiza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma katika kuhudumia wananchi kwa uadilifu.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais alisisitiza kuwa funzo kubwa kutoka kwa hayati Magufuli ni kwamba mustakabali wa Tanzania na Afrika uko mikononi mwa wananchi wake, akihimiza matumizi bora ya rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo endelevu.Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi na wadau wengine, yakilenga kukumbuka mchango wa hayati Magufuli katika ujenzi wa taifa na kuhamasisha kizazi cha sasa kuendeleza misingi ya uzalendo na uchapakazi.





Toa Maoni Yako:
0 comments: