Na Pastor Harris Kapiga.
Uzao Dei;
Changamoto ya KULEA watoto wa KIUME hasa wakifika miaka 12;
1. Baba kuwa mnoko sana ni jambo la kawaida
2. Usiamini kila wanachokwambia Fuatilia kwa karibu mno, wana akili mno; Anaweza kukwambia ameenda Mkesha wa Casfeta kumbe yupo birthday party ya Girlfriend
3. Juwa Marafiki zao, ikiwezekana uwaone! Tembelea home kwao
4. Kama wanasimu zao, ZIARA ZA KUSTUKIZA kwenye Simu zao fanya Mara kwa Mara
5. Mama Ukiona Babaa ana muwajibisha mwanao wa kiume mwache, kuna kona Baba anazielewa alipita huko, mama huzujui;
6. Kama Mama unalea watoto wa Kiume wewe mwenyewe Daa Mungu akusaidie kwa kweli. Unitafute tuongee kwa kina
7. Ombea watoto wako wa Kiume kila siku.
Sisi kila Jumatano siku Maalumu ya kuwaombea maanake! Duu Mungu ndo anawajua zaidi
8. Kama kijana wako Yupo chuo mbali na wewe.
Kama una ndugu Amtembeleee aone Mazingira yake! Vijana wa kiume wana Uongo mwingiiii..
9. Waoneshe unawaheshimu, Baadhi ya Mambo waache wafanye Maamuzi wao;
10. Huwa wanaangalia una husiana vipi na mama yao, Ukimpenda mama yao! Utawa win kirahisi.
Tukana/ piga mama yao mbele zao, Bifu la Maisha.
Hawatakupenda/ watakuwa wanafiki wakiwa wadogo, Wakiwa wakubwa watalipiza kisasi tu.
11. Semina na wao kuhusu, uwajibikaji, Nafasi zao wakiwa kina baba! Mapenzi kabla ya Ndoa, Kumcha Mungu, Kazi kwa bidii, Usafi wa miili yao;
KULEA INAHITAJI HEKIMA YA KIMUNGU SANA
SIO KAZI RAHISI.



Toa Maoni Yako:
0 comments: