Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.


Sehemu ya viongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivyohudhuria hafla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.


Sehemu ya viongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivyohudhuria hafla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.



Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Dodoma, Julai 26, 2025 – Jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika Jumatano, tarehe 29 Oktoba 2025, kwa mujibu wa tangazo rasmi la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, alitoa taarifa hiyo leo katika hafla ya uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi uliofanyika katika makao makuu ya Tume, Njedengwa jijini Dodoma.

Amesema kati ya wapiga kura waliopo kwenye daftari, Tanzania Bara ina jumla ya wapiga kura 36,650,932, huku Zanzibar ikiwa na wapiga kura 1,004,627. Ongezeko hilo ni la asilimia 26.55 ikilinganishwa na idadi ya wapiga kura 29,754,699 walioandikishwa mwaka 2020.

Aidha, wanawake walioandikishwa ni 18,943,455 sawa na asilimia 50.31, wanaume ni 18,712,104 sawa na asilimia 49.69, na watu wenye ulemavu waliojiandikisha ni 49,174.

Katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, jumla ya vituo 99,911 vya kupigia kura vimetangazwa, kati ya hivyo, 97,349 vitakuwa Tanzania Bara na 2,562 Zanzibar — ongezeko la asilimia 22.49 kutoka vituo 81,567 vya mwaka 2020.

Ratiba rasmi ya Uchaguzi Mkuu 2025 ni kama ifuatavyo:

Agosti 9–27, 2025:
Utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais.

Agosti 14–27, 2025:
Utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani.

Agosti 27, 2025:
Siku ya uteuzi rasmi wa wagombea wa nafasi zote (Rais, Makamu wa Rais, Wabunge na Madiwani).

Agosti 28 – Oktoba 28, 2025:
Kipindi rasmi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara.

Agosti 28 – Oktoba 27, 2025:
Kampeni kwa upande wa Zanzibar (kupisha upigaji kura ya mapema).

Oktoba 29, 2025 (Jumatano):
Siku ya kupiga kura nchi nzima kwa nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani.

Jaji Mwambegele amewataka wananchi na wadau wote wa uchaguzi wakiwemo vyama vya siasa, wagombea, waangalizi, asasi za kiraia na vyombo vya habari kuhakikisha wanazingatia sheria, taratibu na miongozo itakayotolewa na Tume ili kuweka mazingira ya uchaguzi huru, haki na wa amani.

“Huu ni uchaguzi wa kihistoria kwa Tanzania. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anashiriki kikamilifu kwa kuzingatia maelekezo ya kisheria,” alisema Jaji Mwambegele.


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: