Na Mwandishi Wetu – Dodoma.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea na mchakato wake wa ndani wa kuwachuja wagombea wa nafasi za ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo orodha ya awali imebainisha jumla ya wabunge 27 wa sasa kutoka majimbo mbalimbali ya Tanzania Bara ambao hawakuteuliwa kuendelea katika hatua ya kupigiwa kura za maoni.
Wabunge hao ni miongoni mwa wale waliokuwa wakihudumu katika majimbo yao kuanzia mwaka 2020 lakini sasa hawakupitishwa katika hatua ya awali ya mchujo, hali inayoashiria mabadiliko makubwa ndani ya chama kuelekea uchaguzi ujao.



Toa Maoni Yako:
0 comments: