Muandaaji wa Muziki nchini Tanzania, Producer Pancho Latino almaarufu Mafia (Pichani) ambae alifanya kazi kwenye studio mbalimbali aliyefariki jana kwa kuzama kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam anatarajia kuzikwa Wilayani Gairo, Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Msanii Fid Q katika ukurasa wake wa Twitter imesema kuwa Marehemu Pancho Latino itahitimishwa siku ya Jumamosi Oktoba 13, 2018 nyumbani kwao.
Ibada itaanza saa 4 asubuhi, na baadae wataaga mwili wa marehemu na maziko yatafanyika saa nane mchana.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: