Wamama / Wadada tuombeeni sana wakaka ....Hasa wale mnaodhani wanawahusu... yaani kaka yako / ndugu au hata yule jamaa unaempenda penda unawaza atakuja kua mumeo... KUNA HATARI KUBWA SANA KIZAZI CHA WANAUME KUPOTEA WAKABAKI WAVULANA... 

Hatari sana kuona wanawake wanajituma (masomoni/ biasharani / kwenye mambo ya Mungu ) Halafu wanaume wamekaa wanatafuta majina (fame). 

Ni huzuni kuona mwanaume hawezi kuweka akiba hata ya 1000 buku tu kwa siku ... ila anapiga pamba za hatari, Huzuni sana kuona wanaume wanashindwa kufanya maamuzi... kusema NDIO au HAPANA! 

Huzuni sana kuona mwanaume anashindwa kujijengea misimamo na kuweka vipaumbele vyake na kuvisimamia, NI HATARI SANA KUONA MWANAUME ANASIFIA SIFIA WATU ILI APATE NAFASI FULANI.

Najua kuna watu mnasoma huu ujumbe na unaona kila kinachotajwa hapa ndio sifa za mchumba wako ... Na kimsingi hata wewe unaona kinachokuweka kwenye hayo mahusiano ni vile unampenda tu na namna ambavyo unahamu ya kuolewa....Ila mpaka kuna wakati unajiuliza mmmh ... Sasa uko mbele itakuaje dadaaaa Fanya maamuzi .

Kuna wakati nilikua naongea na Baba yangu jambo fulani... nikawa najitetea nasema nikifikia hiyo level nitabadilika... akaniambia hapana jitahidi badilika sasa.

Hivi ulivyosasa ndio picha ya baadae... ukishindwa sasa baadae hautaweza. Najua kuna watu moyoni taa nyekundu imekuwakia juu ya hapo mahali ulipo unajipa moyo unasema atabadilika... mmmh sijui !

Mpenzi dada yangu ni bora uolewe na mwanaume... hata kama hana muonekano mzuri, hajui kuvaa vaa ... au wakati mwingine hata kazi yake sio nzuri kiivyo ila unaona ana juhudi fulani ndani yake unaona anandoto fulani na anamipango inayotekelezeka... Kuliko kuolewa na haka kavulana ka handsome kana swagga maarufu ... ILA KANA MANENO MENGI UTENDAJI MDOGO... haka utajuta maana ipo siku katataka ukanunulie shati usiponunua kanakutishia kanasema mimi ujue napendwa na watu wengi sana... wewe una bahati kunipata... SHAAAAME ON YOU BOY !

Wenye muonekano na wakawa wachapakazi ni wachache sana... ukikapata kashikilie kweli... kaombee!

Niwashauri tu kina dada ..ule muda mnaotumiaga kuomba / kuliaaa ili uchumbiwe uolewe... wekeza huo muda kumuombea mtu wako asimame kwenye nafasi yake ! Mumeo yupo tu ila omba kabla hakafika kwako awe ametoka kwenye uvulana awe mwanaume pengine hata kuchelewa kwake uvulana ndiyo unamsumbua.

Ni huzuni.

Na Mtumishi Fred Msungu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: