Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanaume wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanawake wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia na kukata keki ya pamoja
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kilishwa keki na mmoja wa wafanyakzi wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amewataka wanawake mkoani iringa kujifunza kujitegemea katika maisha kutokana na benk nyingi kutoa mikopo yenye riba ndogo ambayo inawasidia kuwainua kiuchumi.
Akizungumza na wafanyakazi wa benk ya NMB tawi la mkwawa Kabati alisema kuwa benk hiyo imesaidia kuinua maisha ya wanawake kwa kuwawezesha mitaji ya kufanyia biashara mbalimbali.
“Mimi nimeshuhudia mara kwa mara mkiviwezesha vikundi vingi vya wanawake ambavyo mmesaidia kukuza maendeleo ya wanawake wa mkoa wa Iringa na ndio maana wanawake wengi wamekuwa wakitoa ushuhuda mzuri juu ya huduma za nzuri za benk hii” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuwa nguzo ya uchumi kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inataka nchi kuwa ya viwanda hivyo wanawake wasiogope kukopa kwenye benk ya NMB kwa kuwa inamashariti nafuu.
Naye meneja wa benk ya NMB tawi la mkwawa George Mwita alisema kuwa bank hiyo imekuwa ikiwawaezesha wanawake kwa kuwapatie elimu ya ujasiliamali na kuwapatia mikopo yenye riba ndogo.
“Sisi kama NMB benk tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana na wanawake kwa kuwa tunajua wanauwezo mkubwa wakufanya biashara ndogo ndogo na zile kubwa” alisema Mwita
Mwita aliwataka wanawake kufika kwenye benk ya NMB ili kujua huduma ambazo zinatolewa na benk hiyo ambayo ipo kila mahali kwa ajili ya kukuza uchumi wa wanawake na wanaume kwa kuwa benk hiyo haichagui mtu bali inawawezesha wananchi wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: