Mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha ametoa ya Moyoni kwatika ukurasa wake wa Facebook:-

"Naona navumilia lakini nashindwa naona kila kukicha habari zinaendelea kutlend tu ni vema ukasikia jambo kutoka kwa muhusika yani mie mwenyewe kuliko kuandika uongo kwa faida yako ili upate folowazi kwenye akaunti yako au ufanikishe malengo yako ya uongo na kuuza magazeti sio sawa kabisa.

Ninachosema ni kwamba huyo Agnes mie sio mpenzi wangu kabisa wala sina mahusiano nae kabisa yoyote yale ila ninachofahamu yeye ni shabiki yangu anayenikubali kama ambavyo unanipenda wewe hivyo kama alipost picha yangu kwenye akaunti yake nadhani alipost kwa upendo wa kuonyesha ni mtu anayenikubali yeye, sio kitu kibaya ila mie sio mtu wangu wala hatutegemei mtoto wala nini kwanza sijawahi kuonanae. 

Mwisho sina mpenzi kabisa wala sina Mahusiano na mwanamke yeyote yule kabisa niamini ninachoongea mie na kama ikitokea Mungu amenipa neema ya kuwa na mtu basi sitaweza kukanusha nitaweka wazi ili hata yeye mhusika ajivunie mie namaliza kwa kusema nimechoka kuandikwa kila mara nipumzisheni na habari zenu za uongo zenye lengo la kumchafua mtu.

SINA MAPENZI NA MTU WALA MAHUSIANO NA YEYOTE YULE NAJIHESHIMU SANA...

Hayo ndiyo ameyaandika mwimbaji Emmanuel Mbasha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: