Miili ya wanajeshi hao ikishushwa kwenye ndege.
Miili ya askari hao ikipelekwa kwenye gari ili kwenda kuhifadhiwa hospitali.
Miili ikipelekwa kwenye gari.
Askari wakibeba miili ya askari wenzao.
Miili hiyo imepokelewa na Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo.
Ndege ya UN iliyokuwa imebeba miili hiyo.
Maofisa wa JWTZ waliofika kupokea miili hiyo.

MIILI ya Askari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi wakilinda amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imewasili nchini leo, Jumatatu, Desemba 11, 2017 saa 12 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.

Miili hiyo imepokelewa na wanajeshi wenzao, ndugu, marafiki, jamaa na mamia ya wananchi waliojitokeza katika Uwanja huo jioni hii ambapo itaagwa Alhamisi, Disemba 14 katika Viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.

Wanajeshi hao waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo wanajeshi wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa.

Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo. Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: