Baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) kumwimba Mzee Onyango kuwa zilipendwa sasa mzee huyo ameibuka na kukana kuwa yeye sio Zilipendwa.
Hatimaye Mzee Onyango ambaye ni Mwigizaji Mkongwe nchini Tanzania amemjibu Diamond Platinumz kwa vitendo baada ya kuachia filamu yake mpya ya iitwayo BABU
THE PERFECT MAN kupitia kampuni yake ya ONYANGOPRODUCTION.
"Nashangaa sana kusikia Diamond Platinumz kuimba kwamba mimi na Mzee Jangala zilipendwa, mtoto huyu amenikosea sana mimi bado napendwa na mashabiki zangu bado wanaamini kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi ya uigizaji bila tatizo lolote" alisema Mzee Onyango.
Toa Maoni Yako:
0 comments: