Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya.
Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari).
Kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Lipesi Kayombo na Afisa Utumishi wa manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma akishauri jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo.
Usikivu ni jambo la busara kikaoni.
Na Mathias Canal, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Lipesi Kayombo ameshauri wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao kwa kuwatumikia wananchi kwa haki.

Kayombo aliwasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Mitaa.

Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo wenyeviti wote wamekabidhiwa Bendera, Rejista, Vitini vyenye miongozo ya kisheria sambamba na vitini vinavyobainisha majukumu ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kutoingiliana katika utendaji na viongozi wengine wakiwemo watendaji wa Mitaa na Kata.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa wenyeviti wanapaswa kuwasimamia vyema wananchi kulipa kodi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya Manispaa kujisimamia yenyewe na kujiendesha kirahisi.

Mstahiki Meya ametumia Kikao hicho kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg John Lipesi Kayombo kwa uongozi wake imara na uliothubutu kwani umewafanya wananchi katika Manispaa hiyo kuwa walipaji wazuri wa kodi.

Jacob amesema kuwa mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya mfano na kuzishinda Manispaa zingine katika Jiji la Dar es salaam.

Kuhusu Posho za wenyeviti wa Mitaa, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewasihi wenyeviti kuwa na subira kwani wanaandaa mpango imara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuwalipa malimbikizo ya posho zao zote wanazodai.

Pia amewasihi wenyeviti hao kutumia Uhuru wao kikatiba kuwafungulia kesi wale wote wanaowaonea, kuwazalilisha na kuwakejeli kwa kuwafungulia kesi katika mahakama kwa mujibu wa sheria.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: