Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akimlisha keki mke wake.
Mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akikabishi keki kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwa ajili ya meza kuu
Hapa ni ndani ya ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga ambapo usiku wa Ijumaa Machi 3,2017 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanya sherehe ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 pamoja na kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na maafisa wa polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema Machi 3 kila mwaka huwa ni siku ya Polisi ‘Police Family Day’ ambapo pamoja na kuadhimisha siku hiyo,jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeamua kuwafanyia sherehe ya kuwaaga wastaafu 10 wa jeshi hilo sambamba na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.
“Tumeanza sherehe hizi kwa mkuu wa mkoa kukagua gwaride katika uwanja wa Shycom lakini pia kutoa tuzo kwa askari na wadau waliofanya kazi vyema mwaka 2016 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga”,alisema kamanda Muliro.
Naye Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack alitumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na sasa vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa sherehe hizo ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri ukumbini.
Ijumaa Machi 3,2016 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga-Aliyesimama
ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
akizungumza wakati wa kufungua sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la
polisi na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.Kulia ni mgeni
rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.Kushoto ni mke wa kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Mama Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwaomba wadau wote wa ulinzi na usalama kuungana na jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha amani ya mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza ukumbini
Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Dayosisi ya Shinyanga, Dkt. John Nkola akiwasalimia wageni mbalimbali
Viongozi wa migodi na benki mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Wadau wa ulinzi na usalama wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wastaafu wa jeshi la polisi wakiwa wamekaa ukumbini.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akiwasalimia wadau walioshiriki sherehe hizo.Kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Annamaria Yondani.
Askari wa jeshi la polisi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde akigonga cheers na mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
Wadau wakiwa ukumbini.
Sherehe inaendelea.
Zoezi la kukabidhi zawadi kwa wastaafu wa jeshi la polisi linaendelea
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Mstaafu akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Sherehe inaendelea.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwapa zawadi wastaafu wa jeshi la polisi.
Wadau wakiwa ukumbini.
Kamati ya maandalizi ya sherehe wakijitambulisha ukumbini.
Meza kuu na wadau wakicheza muziki ukumbini.
Muziki unaendelea
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: