Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli nne kwa ajili ya wanafunzi wa kike waliofanya vyema katika mitihani yao ili ziwasaidie kurahisisha usafiri kufika shuleni lakini pia baiskeli moja kwa ajili ya mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule hiyo.
Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Bulyanhulu, mwalimu Bumi Mwasalujonja.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 baada ya kupata daraja la kwanza.
Wanawake kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiwa na wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika mtihani.
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidh baiskeli kwa mwalimu wa nidhamu/mlezi shule ya sekondari Bugarama Prisca Mwanantemi.
Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao pamoja na mwalimu wao wakiwa wameshikilia baiskeli zao.
Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8, 2017.
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Muuguzi kituo cha afya Bugarama Mwalushani Mabula.
Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno.
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya ,Dkt. John Malongo kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho
Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Lunguya.
Kulia ni Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya, Dkt. John Malongo akiwaaga wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu.
Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakifurahia baada ya kumaliza ziara yao.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.
---
Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.
Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.
Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.
“Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.
“Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”, aliongeza Senkondo.
Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: