Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akikabidhi Tsh milioni moja kwa Mpoki Ibrahim ambaye ni mshindi wa mbio za kilomita kumi kwa walemavu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zinazodhaminiwa na GAPCO Tanzania zilizofanyika Moshi hivi karibuni. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair.
Washindi wa mbio za Kilimanjaro Premium lager Marathon za kilomita 10 kwa walemavu zinazodhaminiwa na GAPCO Tanzania wakiwa wameshikilia mfano wa hundi ya Tsh milioni moja walizoshinda kila mmoja. Kutoka kushoto ni Charles Mihambo aliyeshinda mbio za wanaume wanaoendesha baiskeli za kunyonga kwa mikono, Voster Peter-mbio za baiskeli za magurudumu mawili kwa wanaume, Sophia Mkenda-mbio za baiskeli za magurudumu mawili kwa wanawake na Mpoki Ibrahim-mbio za baiskeli za kunyonga kwa mikono kwa wanawake.GAPCO yapongezwa kwa kuimarisha mbio za walemavu
Na Mwandishi wetu
Baadhi ya washiriki wa mbio za kilomita 10 kwa walemavu zinazodaminiwa na GAPCO Tanzania, wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwajali walemavu na kuhakikisha wanafanya vizuri katika riadha.
Pongezi hizi zinakuja siku chache baada ya kumalizika kwa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambapo GAPCO iliwadhamini washiriki zaidi ya 90. Washiriki kutoka Dar es Salaam walilipiwa malazi,chakula na usafiri na wale kutoka Moshi na Arusha walilipiwa usafiri.
Mshindi wa mbio za baiskeli ya kunyonga kwa mikono kwa wanawake, Mpoki Ibrahim, alisema GAPCO wameweza kufanya jambo ambalo makampuni mengine yameshindwa. “Wametufanya tujiskie fahari kwani tunajua jinsi gani ni ngumu kuwasafirisha watu wote hawaw enye ulemavu lakini GAPCO wamefanya jambo la kipekee,” alisema.
“Hii ni mara yangu ya pili kushiriki mwaka jana nilikuwa mshindi wa tatu lakini nashukuru mwaka huu nimekuwa wa kwanza na nimejishindia Tsh milioni moja. Fedha hizi nitatumia kutunisha mtaji wa biashara yangu pale Machinga Complex Karume. Nitaongeza mtaji wangu wa maji na ninachoomba tu ni kuwa GAPCO waendelee kutudhamini mwakani,” alisema na kuyaomba makampuni mengine yaige mfano huo.
Alisema siri ya mafanikio yake ni mazoezi ya kutosha kwani yeye huendesha baiskeli yake kila siku kutoka Vingunguti hadi Karume. “Hili ni zoezi tosha kwangu na ilinisukuma kujisajili kushiriki Kilimanjaro Marathon kwani uwezo nilikuwa nao na pia nilikuwa na pumzi ya kutosha mabayo iliniwezesha kumudu mbio hizo,” alisema.
Kwa upande wake mshindi upande wa wanaume wanaoendesha baiskeli za kunyonga kwa mikono, Charles Mihambo, aliimwagia GAPCO sifa kwa kutumia sehemu ya mapato yao kuwajali walemavu. “Watu wengine hawaoni faida ya kufanya hivyo lakini GAPCO wamedhamini mbio za walemavu kwa miaka saba sasa jambo ambalo linatupa faraja sana,” alisema.
Alisema hii ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki mbio hizi na kilichomsukuma hasa ni udhamini wa uhakika wa GAPCO na pia alikuwa anafanya mazoezi kila siku Tabora, jambo ambalo lilimpa ari ya kushinda.
“Milioni moja niliyoshinda nimeshamtumia mke wangu Tabora nikisharudi tutakaa tupange tufanye nini kwani mimi ni mkulima na mfanyabiashara pia kwa hivyo tutawekeza katika mojawapo ya shughuli hizi,” alisema huku akiipongeza timu yote ya GAPCO kwa kufanikisha mbio hizo za kilomita 10.
GAPCO Tanzania ilitoa jumla ya Tsh milioni 10.4 kwa ambazo ziligawiwa kwa washindi wa mbio hizo.
Wadhamini wengine wa Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42 km, Tigo 21km. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Toa Maoni Yako:
0 comments: