
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua rasmi utoaji wa Fidia kwa Wafanyakazi waliopatwa na madhara ya kiafya mahali pa kazini. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. Wengine pichani ni Manaibu wakeKulia kwake ni Naibu wake, Dkt. Abdallah Possi na Mh. Anthony Mavunde, Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya WCF, Emmanuel Humba, (wane kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Masha Mshomba.( Picha na Muhidin Sufiani)


Waziri Mhagama akihutubia

Mwenyekiti wa bodi ya WCF, Bw. Emmanuekl Humba akitoa hotuba yake

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, akitioa hotuba yake.

Mgeni rasmi, manaibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi wa WCF, na waliotunukiwa vyeti wakiwa kwenye bpicha ya pamoja.

Waziri Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi Cheti cha utoaji huduma bora za afya, Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Muhimbili Orthopaedic Institute’ Dkt. Othman Kiloloma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam.
---
Na Muhidin Sufiani, Dar.
SERIKALI
imewaagiza Waajiri wote nchini kuwasilisha kwa wakati michango ya mafao
ya fidia kwa wafanyakazi ili kuwawezesha watumishi wao kupata huduma za
matibabu pindi watakapoumia au kuugua wakiwa katika maeneo yao ya kazi.
Agizo
hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Ulemavu) Jenister Mhagama
wakati alipokuwa akizindua huduma za utoaji wa mafao ya fidia na ubia
baina ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na watoa huduma za afya
nchini.
Mhagama
alisema suala la uchangiaji wa mafao hayo sio la hiari ila lipo
kisheria na hivyo ni wajibu wa waajiri wote nchini kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wao wanaingizwa katika mfumo huo ili kuwawezesha wafanyakazi
kuwa na uhakika wa kulipwa fidia pindi wanapokuwa kazini
“Katika
mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imelipa michango yote ya wafanyakazi
wake, na huu ni mfano unaopaswa kuigwa na waajiri wengine nchini, na
natoa rai kwa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la
Wafanyakazi nchini (TUCTA) linasimamia suala hili” alisema Mhagama.
Aidha
Mhagama alisema lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo wa wafanyakazi nchini
ni kusaidia kutatua kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi wa sekta za
umma na binafsi, ambao wamekuwa wakilalamikia huduma hafifu zinazotolewa
pindi wapatapo majanga mbalimbali wakiwa kazini ikiwemo ajali na vifo.
Waziri
Mhagama alitaka Bodi ya mfuko huo kusimamia kikamilifu utekelezaji wa
sheria zilizopo ili kuhakikisha kuwa waajiri wote hususani wa sekta
binafsi wanawasilisha michango kwa wakati.
Akifafanua
zaidi Waziri Mhagama aliuataka mfuko huo kujitangaza zaidi kwa sekta
zisizo rasmi ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi hususani wa kipato cha
chini kujiunga na mfuko huo na kuwasaidia kufaidi huduma zinazotolewa.
“Natoa
rai kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii nchini ikiwemo wa WCF
mjitangaze katika sekta zisizo rasmi ikiwemo waendesha bodaboda, akina
mama lishe, kwa kuwa idadi yao ni kubwa na hiyo itawezesha kupata
wanachama wengi zaidi” alisema Mhagama.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Masha Musomba alisema hadi
kufikia sasa mfuko huo umeweza kutoa usajili wa waajiri 5945 pamoja na
kuendesha mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo watumishi wa mfuko huo
ikiwemo madaktari.
Aidha
Musomba anasema pia mfuko huo umeingia ubia na taasisi 7 za utoaji
huduma za afya nchini, ambazo ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Kansa ya Ocean Road.
Musomba
anazitaja taasisi nyingine kuwa ni Strategis, AAR, mfuko wa Jubilee, na
Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo taasisi hizo zinazoendelea
kushughulikia kesi 189 zilizolipotiwa katika mfuko huo.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Aggrey Mwinuka alisema
mfumo huo wa fidia umekuja katika wakati muafaka kwa kuwa sheria
zilikuwepo katika vitabu na hazikuwa na utekelezaji uliokusudiwa.
Mwinuka
alisema ili kuhakikisha kuwa malengo ya mfuko huo yanatekezeka ni
wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa inafanya majadiliano ya mara kwa
mara na waajiri ili kuangalia viwango vya makato ya michango ya
wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya mfuko huo, Emmanuel Homba alisema uwekaji wa mfumo wa mafao
ya fidia utawezesha wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi
kuchangia kikamilifu katika Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ujenzi
wa uchumi wa viwanda nchini.


Toa Maoni Yako:
0 comments: