Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dk.Natu Mwamba hapa akisikiliza Risala toka kwa mkuu wa mafunzo alipokuwa akielezea kuhusu idadi ya wahitimu na changamoto zinazokabili Taasisis kwa sasa ikiwemo kuiomba Serikali kuendelea kusaidia kadri ya uwezo wake ili Taasisi hiyo iweze kufikia Malengo ya kutoa mafunzo ngazi ya Shada ya uzamili (Masters).
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dk. Joseph Kihanda (katikati akiskiliza kwa makoni Brass Band ambapo yeye kama mkuu wa Taasisi ameelezea Mengi aliyoyafanya kwa Muda mfupi aliokaa katika Taasisis hiyo ikiwemo kutoa Fursa kwa wafanyakazi wengi zaidi kujiendeleza kimasomo hasa ngazi ya Masters na PHD Ambapo hadi sasa waalimu wapatao 12 wanasoma PHD katika hatua mbalimbali,Amejitahidi kuboresha Miundombinu ikiwemo Madarasa ya Kisasa na Ujenzi wa jengo jipya la Ghorofa 6 litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zadi ya 3,000 kwa mara moja na mengine mengi.
Waadhiri Mbalimbali Akiwemo Mr Msabi, Dk.Aniceth Mpanju ,Mr Justin ,Mr Marobe na Mr Bajjet nao wakiskiliza kwa umakini wakati mahafali yakiendele
Wahitimu mbalimbali wakifuatilia kwa umakini
Wahitimu wa Shahada ya Ugavi na Manunuzi (BPLM )Bwana Hazrat Mandamo akifurahia jambo na Bi. Rosalia Kisongo wakifurahia kwa pamoja baada ya Kuhitimu leo
Mhitimu wa Shahada ya Ugavi na Manunuzi (BPLM ) Bi. Radia akifurahia kwa pamoja na wenzake wa Shahada ya Uhasibu (BAC) baada ya Kuhitimu leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: