Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya EQUATOR SUMA JKT Co. Ltd. Kiwanda kitakachokuwa kinatengeneza magari ya Zimamoto na Matrekta hapa nchini, Ndg. Robert Mangazeni akitoa maelezo jinsi ya kiwanda hicho kitakavyofanya kazi alipotembelewa na Naibu Kamishna Jenerali pamoja na Viongozi waandamizi wa Jehi hilo.
Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi lka Zimamoto na Uokoaji Lidwino Mgumba, wa pili kushoto akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Equator Suma JKT Co. Ltd Ndg. Robert Mangaza wa kwanza kulia, wakati akitoa maelezo ya jinsi gani mitambo ya kufunga magari hayo ya zimamoto yatakavyotengenezwa.
Moja ya gari la Zimamoto ambalo litatengenezwa na kampuni ya Equator Suma JKT Co. Ltd baada ya kiwanda hicho kuanza kufanya kazi. (PICHA NA FC GODFREY PETER)
Picha ya pamoja.

Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lidwino Mgumba pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo wametembelea kiwanda kinachotarajiwa kutengeneza magari ya Zimamoto na Matrekta (EQUATOR SUMA JKT Co. Ltd) kilichopo Ruvu eneo la Mlandizi mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo ambayo aliifanya mapema leo asubuhi, Naibu Kamishna Jenerali alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Mangazeni na kufanya mazungumzo ya kuona ni jinsi gani wanaweza kutatua tatizo la kukabiliana na majanga ya moto hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo alimuakikishia Naibu Kamisha Jenerali “kiwanda hiki kitakapo zinduliwa tutaweza kumaliza changamoto za uchache wa vitendea kazi inayolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji“ Alisema Mkurugenzi huyo.

Naye Naibu Kamishna Jenerali alishukuru pamoja na kumuahidi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo “tutashirikiana kwa karibu na kwa kitaalamu kwani sisi ndiyo wenye dhamana ya kuokoa maisha na mali za umma wa watanzania katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani pamoja na majanga mengine“ Alisema Naibu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: