Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na jeshi hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Na BMG
Makale ameeleza kwamba mtuhumiwa huyo
alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha shilingi 240,000 kati ya
shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa mmoja wa walioomba
kujiunga na JWTZ.
Amebainisha kwamba mtuhumiwa mmoja
ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha amekuwa akimsaidia
mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga
na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa amekuwa akihitaji
kiasi cha shilingi 500,000.
Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.
"Kitendo
cha mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo
chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo
jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa
wakili wa serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.
Aidha
Makale ameongeza kwamba TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha
mahakamani Katibu wa Idara ya Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa
kosa la tuhuma za kupokea rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki
Mgaya ili asimchukulie hatua za kinidhamu kazini.


Toa Maoni Yako:
0 comments: