Na Mwandishi Wetu, Dar esSalaam.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini.
Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla.
Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Akizungumza wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati.
Alisema kwa wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao, huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita, kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita,kulia akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi,wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni Thabit Mndeme, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani mteja wao Hassan Omary Hamis, jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhi hati ya kiwanja kwa Hassan Omary Hamis
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akizungumza jambo wakati anakabidhi hati za viwanja kwa wateja wao wa Bayport Financial Services hawapo pichani leo jijini Dar es Salam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: