Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga leo  wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.

Akishinda urais Dk Magufuli amehidi kujenga barabara ya lami kutoka Soni  hadi Bumbuli yenye umbali kwa Km 22. Pia ameahidhi kuharakisha mchakato wa kukikabidhi kiwanda cha chai cha Mponde kwa wananchi na kuanza kuzalisha.

Pia ameahidi kuboresha hali za wanajeshi, walimu na wafanyakazi nchini

Dk Magufuli ambaye kampeni zake huzifanya kwa magar, tayari hadi sasa kafanya  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Morogoro na Tanga na kesho anaanza kampeni katika Mkoa wa Mara.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Sehemu ya umati wa wananchi ulifurika kwenye mkutano huo wa kampeni katika Jimbo la Bumbuli.
 Dk Magufuli akiwa amembeba mtoto huyo baada ya kufurahishwa na uimbaji wake katika mkutano wa kampeni Kata ya Malamba, Wilaya ya Nkinga leo

 Mmoja wa wazee wa Kata ya Malamba akiwa na furaha baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli.


 Wakiwa na furaha ni Dk Magufuli ( katikati), Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, Januari Makamba na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Shekifu walipokuwa wakiangalia kikundi cha uchekeshaji cha The Comedy Orijino wakati wa mkutano

 Msanii Joti wa kikundi cha uchekeshaji cha The Comedy Orijino akimchukua Dk Magufuli ili ajumuike nao kucheza muziki wakati wa kampeni hizo.

 Dk Magufuli akijumika kucheza muziki na wasanii wa kikundi cha The Comedy Orijino

 Baadhi ya wazee wa Kata ya Malamba, mkoani Tanga, wakiwa na picha za  Dk Magufuli

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Nkinga

 Baadhi ya vijana wakishangilia baada Dk, Magufuli kutoa ahadi kuwa akishinda Serikali yake itakuwa inatoa kwa kila kijiji sh. mil 50 kwa wazee na vijana kwa ajili ya mikopo ya kuanzishia miradi ili wajikimu kimaisha.

 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika Kijiji cha Mashewa

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la  Korogwe  Vijijini, Steven Ngonyani 'Profesa Maji Marefu"

 Akimpunia mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli.

 Mfuasi wa CCM akishangilia kwa furaha baada Mgombea urais, Dk Magufuli kuahidi kwamba akishinda wataanzisha    utaratibu wa kuwakopesha wanawake na Vijana kwa kila kijiji kupatiwa shmil 50. Mkutano huo wa kampeni umefanyika katiuka Kata ya Matalawanda.

 Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi, mgombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani



 Wafuasi wa CCM wakiwa wameshikilia bango hilo katika mkutano wa kampeni mjini Korogwe



Dk magufuli akijinadi kwa wananchi katika mji wa Mombo


 Katibu Mkuu msitaafu, Yusufu Makamba akielezea sifa lukuki alizonazo Dk Magufuli tofauti na mgombea kupitia Umoja wa Katiba ya wananchi

 Dk Magufuli akiteta jambo na January Makamba

 Wasani wa The Comedy wakilishambulia jukwa wakati wa mkutano huo



 Mwakilishi wa watu wenye ulemavu Amon Mpanju akielezea jinsi CCM inavyo wajali watu wa namba hiyo wakati wa mkutano mjini Lushoto leo



 Dk Magufuli akimtambulisha kwa wananchi Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba

 Wagombea udiwani Jimbo la Bumbuli wakitambuliwa kwa wananchi katika kkiutano huo

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu akimnanga Frederick Sumaye kwa ni fisadi zaidi ya Lowassa.

 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mlalo, Hassan Ngwilizi akimpigia chapuo Dk Magufuli katika mkutano huo.

 Mjumbe wa Kamati ya kaampeni ya CCM, Ummy Mwalimu akimpigia debe Dk Magufuli wakati wa mkutano huo
Dk Magufuli akijinadi mjini Lushoto
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: