Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa ( Kushoto)
akimkabithi kikombe Afisa masoko na biashara wa Airtel , Emmanuel
Raphael mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
mshindi wa pili katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ya
mwaka huu. Katika maonyesho hayo Airtel ilipata makombe manne katika
vipengele mbalimbali ikiwemo, Mtoa huduma bora, Mtoa huduma bora katika
sekta ya mawasiliano, ubora katika mawasiliano ya habari na tecknologia
pamoja na mshindi wa pili wa maonyesho kwa mwaka huu. Akishuhudia
(katikati) ni mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Commerce , Industrial
and Agriculture Elibariki Mmari.
Afisa masoko na biashara wa Airtel, Emmanuel Raphael katika picha na
makombe mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika
Mashariki ya mwaka huu.
Wafanyakazi wa Airtel kwa pamoja wakiwa na makombe yao mara baada ya kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu
Toa Maoni Yako:
0 comments: