Na Matukio daima blog.

CHAMA Cha ACT wazalendo kimewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu waliojitokeza kuomba kuchaguliwa kupokea  nafasi ya  aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kwa  madai kuwa hapaswi tena kupewa kura katika jimbo hilo.

Katibu Wilaya  wa ACT wazalendo Wilaya ya  Iringa Bw Zhenepa Ally leo wakati  wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Chiku  Abwao (ACT - Wazalendo) kwenye kata ya Kitwiru .

Alisema kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa wakati  wa Ubunge wake awali alikuwa akipambana na ujangili kwa kupambana na  wauwaji wa Tembo na kila mkutano wake alikuwa akionyesha kupiga vita  ujangili ila baada ya kushikamana na Waziri Lazaro Nyalandu (CCM) kwa  kusafiri pamoja katika Ziara za nje aligeuka ghafla na kuacha kabisa  kuzungumzia ujangili.

Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu.  Waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge jimbo hilo ambalo Mchungaji  Msigwa kashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Ubunge ambao wananchi wanapaswa  kuwachuja kuwa ni Chiku Abwao (ACT Wazalendo), Frederick
Mwakalebela (CCM) na Daud Masasi (ADC) na sio kupoteza kura kwa kumpa tena mchungaji Msigwa ambae ametelekeza jimbo hilo kwa miaka yote mitano.

" Katika uchaguzi huu wananchi wa Iringa tunaomba muwapime watu watatu waliojitokeza kumpokea Ubunge Mchungaji Msigwa"

Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo hilo la Iringa Mjini Bi  Abwao alisema jimbo la Iringa Mjini ni moja kati ya majimbo ambayo yalikuwa rahisi  zaidi upinzani kuendelea kuongoza tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ila kutokana na kushindwa kwa Mchungaji Msigwa jimbo hilo wananchi  wamepoteza imani na upinzani.

Abwao aliwaomba wananchi wa jimbo la Iringa mjini kumchague yeye kuwa mbunge wao kwani sera nzuri za kuwakomboa wananchi hao

" Mbunge Msigwa aliahidi kuwapa nyavu kwa maana ya mitaji ila kipindi
chake chote kaishia kufanya mikutano ya vurugu na kutukana wananchi wake kuwa ni wavivu wanaopenda kucheza bao wakati nae ni miongoni mwa wavivu hao na wacheza bao wazuri"

Hivyo alitaka wananchi wa jimbo la Iringa ili kurejesha heshima ya upinzani  jimbo la Iringa Mjini ni wakati wa kuchagua chama cha ACT Wazalendo kuanzia Udiwani Ubunge na Urais na sio Chadema kupitia mwamvuli wao wa  Ukawa ambao wamesimamisha mgombea ambae yupo katika orodha ya mafisadi.

Akizungumzia kuhusiana na Mgombea Urais wa Ukawa Chiku, alisema kuwa Mgombea huyo  hana sifa ya kuwakomboa watanzania kwani ni genge la walanguzi  linalotaka kwenda kutumia Ikulu kwa kurejesha mamilioni ya pesa waliotumia kununua Ikulu.

Hata hivyo alisema watanzania wasidanganyike na safari ya matumaini ya Ukawa kwani safari hiyo haipo tena na hivyo ni vema kuchukua hatua kwa
kukataa wagombea hao wa Ukawa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: