MHAMASISHAJI na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo ndani ya ofisi za Global Publishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar katika uzunduzi maalumu wa vitabu vyake vitatu, Shigongo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusoma vitabu ili kupata maarifa mengi ya juu ya mafanikio maishani.
“Kila mmoja ana ndoto za kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kuondoka mahali alipo. Wengi hushindwa kupiga hatua za mafanikio maishani kwa sababu nyingi yakiwemo mazingira waliyokulia wakiaminishwa kuwa hawawezi kufanya chochote maishani, jambo ambalo si la kweli kwani kila mmoja anaweza kufikia ndoto zake akiamua tu kubadili fikra na namna ya kutenda mambo maishani,” alisema Shigongo.
Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Uzinduzi wa vitabu hivyo ni kuashiria kwake kuingia rasmi mitaani na kusambazwa kwenye kona mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo vinatarajiwa kubadilisha maisha ya maelfu ya wasomaji watakaofanikiwa kupata siri za mafanikio.
(PICHA: MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)


Toa Maoni Yako:
0 comments: