Aliyekuwa mbunge Ludewa kati ya mwaka 2002- 2005 Bw. Stanile Kolimba akieleza ubora wa mbunge wa sasa wa Ludewa Deo Filikunjombe na wabunge waliopita.
Mkazi wa kijji cha Lupanga akilia kwa furaha baada ya mbnge wao Filikunjombe kuwasaidia kitanda cha kujifungulia wakati awali walikuwa hawana.
mwenyekiti wa kijiji cha Lupanga akiwa amepiga magoti juu ya mezi kumpongeza Filikunjombe kwa kazi nzuri.
| Filikunjombe akisalimiana na watoto wa shule ya Lupanga. |
Na MatukiodaimaBlog , Ludewa
Aliyekuwa mbunge wa sita toka nchi ipate uhuru katika jimbo la Ludewa, Stanley Kolimba amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa utendaji kazi wake na kuwa mbali ya kuwa amepata kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa nafasi ya ubunge ila hakuweza kufanya mambo makubwa kama yanayofanywa na mbunge wa sasa katika jimbo hilo.
Kolimba alitoa kauli hiyo jana wakati akimshukuru mbunge Filikunjombe kwa kusaidi vifaa mbali mbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 10 katika kijiji cha Lupanga kata ya Lupanga wilaya ya Ludewa.
Alisema jimbo hilo la Ludewa limepata kuwa na wabunge saba hadi sasa toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 ila kazi kubwa inayofanywa na mbunge huyo wa awamu ya saba Bw Filikunjombe hakuna mbunge ambae amepata kuifanya na kuwa kuna haja ya wananchi wa wilaya ya Ludewa na viongozi kumpongeza mbunge huyo kwa utendaji kazi na uwakilishi wa wananchi uliotukuka.
Hata hivyo Kolimba ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa alisema heshima kubwa ya wananchi wa Ludewa kwa sasa imeanza kuonekana kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge huyo na kuwa nguvu ya chama tawala.
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe aliwataka wananchi hao kuendelea kumpa ushirikiano zaidi ili kuweza kuwatumikia na kuwa kuongeza kuwa lengo lake kuona posho anazozipata bungeni kama mbunge zinawanufaisha wananchi wake na si vinginevyo.
Alisema kuwa moja ya ndoto yake katika kuwatumikia wana Ludewa imetimia hivyo kazi kubwa ya wananchi wa jimbo hilo ni kuendelea kumtumia zaidi ili kwa upande wake kuwasaidia pale ambapo wananchi hao wanashindwa.
Katika ziara hiyo mbunge Filikunjombe aliweza kutimiza ahadi yake ya mabati mabati 170, saruji mifuko 200, kitanda cha kujifungulia wajawazito na darubini vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 15.


Toa Maoni Yako:
0 comments: