MSHIRIKI katika TUZO za Msaanii anayechipukia, Denis Albert Katagira maarufu kama ‘AFRO MANIAC’ ameapa kuupandisha chati muziki wa Tanzania katika anga za kimataifa kwa lengo la kuitangaza nchi yake kimuziki na kutoa changamoto kwa mataifa hayo.
Akizungumza kupitia mahojiano yake na mitandao mbalimbali ya kijamii AFRO MANIAC anayetamba na kibao cha ‘Haiko sawa’ amesema lengo lake ni kuona muziki wa kitanzania unazidi kupanda chati na kusisitiza ushirikiano kwa wasanii wote nchini ili kufikia malengo hayo.
Amesema tofauti na miaka ya nyuma hivi sasa muziki wa hapa nchini unazidi kukua siku hadi siku kutokana na vijana wengi waliopo kwa ‘game’ hilo kukaza buti, jambo alilosema kuwa linatia moyo na kuleta matumaini kwa watu wengi hasa wapenzi wa muziki huo.
“Kila mtu ukimsikiliza anakaza ili aweze kutoka tofauti na mfumo wa mwenzake, ushindani umekuwa juu ,malengo pamoja na nia ya kweli ndiyo itabadilisha soko la muziki wetu hapa nchini” amesema AFRO MANIAC
Kuhusu ushiriki wake katika Tuzo za Kilimanjaro Music Awards Mwaka huu 2015, kama msanii anayechipukia, AFRO MANIAC amesema imani yake ni kwamba watanzania wameiona kazi aliyoifanya hivyo jukumu la kumpigia kura za kumpa ushindi limebaki mikononi mwao ili aweze kushinda TUZO hiyo.
‘Hakuna ubishi kuwa tuzo zina ushindani mkubwa lakini siku zote kitu kizuri ndicho kitakachopigiwa kura na kuibuka na ushindi katika fainali hizo’alisema AFRO MANIAC aliyepo chini ya usimamizi wa Kampuni ya Biggy Jay Entertaintment Inc.
AFRO MANIAC Kwa sasa yupo UK Birmingham City University anachukua Degree ya BA (Hons) Bachelors in Music Business and Marketing, so yuko very committed na hii tasnia.
Mbali na kibao chake cha "Haiko sawa" kinachotamba kwa sasa pia nyimbo zake kama "Mama Drama" aliomshirikisha Mzee Kasongo wa Kanema, kuna "Waombe Poo", pia kuna "Nishalewa" alioshirikiana na Mchizi Mox na Country Boy zinatamba katika vituo mbalimbali vya Redio na Luninga.
Amewaomba WATANZANIA wote kumpigia kura kwa wingi kupitia Namba zao za simu kwa kutuma ujumbe wa message ukiandika neno hili CC3 Kwenda Namba 15415
Katika mitandao yoyote ile.




Toa Maoni Yako:
0 comments: