Mei 21, 1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao. Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba. Meli ilikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote. Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.

WADAU TUUNGANE KATIKA KUWAOMBEA WENZETU KUANZIA HIVI SASA IKIWA NDIO MUDA MELI ILIANZA SAFARI KUTOKA BUKOBA MJINI KUELEKEA KEMONDO BAY AMBAPO ILIENDELEA NA SAFARI KUELEKEA MWANZA AMBAPO ILIZAMA MUDA MCHACHE KABLA YA KUTIA NANGA JIJINI MWANZA

Mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: