Pichani: Kutokea kushoto ni Mh. Hamad Rashid (Mbunge wa CUF kutoka jimbo la Wawi Zanzibar) na Mh. Kangi Lugola (Mbunge wa CCM kutoka jimbo la Mwibara, Tanzania Bara) Mara nyingi nimekuwa naigomea akili yangu kuamini ya kuwa kitu kizuri na cha kipekee lazima kifanyike na wale wanaoitwa wazoefu (experienced).
Jiulize swali lisilohitaji hata kikokotozi (calculator):
" Hivi wale waliotengeneza ile meli maarufu Duniani kwote iliyofahamika kwa jina la TITANIC walikuwa na hawana uzoefu ? Jibu utapata ni kuwa walikuwa wazoefu tena tuwaite sugu lakini meli waliyotengeneza ilizama.
Hivyo basi usiruhusu sauti ya ndani yako kukuaminisha kuwa huwezi au kuna watu mahsusi kwa jambo fulani ambao wamebobea , ila kumbuka kutumia uzoefu wao pale inapobidi.
Nimeona nikutie moyo kijana ambaye inawezekana ndio kwanza umeanza kazi au una njozi fulani na mane no yahusuyo uzoefu yamekuwa kikwazo kwako.
Nimekuwa katika kazi ninazozifanya kwa miaka 8 sasa ila bado napata kujifunza mambo mapya kila siku kutoka kwa wale tunaowaita wenye uzoefu mdogo.
Songa mbele... mtakutana katika kilele cha mafanikio.
Nawatakieni siku njema yenye baraka tele.
Cheers !!!
@ BAGATECH
Godwin D. Msigwa
Morogoro
Tanzania
26 Mei 2015.



Toa Maoni Yako:
0 comments: