Mabondia Adam Ngange wa Chanika Dar es Salaam (kushoto) na Iddi Pialali wa Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakitupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA). Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita.
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Adam Ngange (kushoto) wa Chanika akimpa kitu roho inapenda bondia Iddi Pialala wa Bagamoyo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA). Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita.
---
Na Mwandishi Wetu.
BONDIA Adam Ngange wa Chanika Dar es Salaam amemsambaratika Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo kwa point katika mpambano wao mkali wa raundi sita uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) ambapo kulikuwa na shamra shamra za kutosha kwa upande wa Pialali.
Ngumi zilianza kupigwa kwa Pialali kwa kumshambulia sana Ngange mnamo raundi za mwanzo rakini kadri mpambano ulivyokuwa unasonga mbele na raundi kuzidi kwenda mbele ndipo Ngange akazinduka na kuanza nae kumshambulia kwa kasi zaidi ambapo mpaka kufika raundi ya sita.
Raundi ambayo ilitawaliwa na ngange kupiga ngumi za misri ya paka anavyopiga kibao na kurudisha mkono alipo utoa mpaka raundi ya mwisho ya mchezo Ngange alikuwa mshindi kwa point mbili zaidi ya Pialali akika lilikuwa pambano zuri ambalo lilikusanya mashabiki wengi wa mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Mpambano huo ulileta raha zaidi baada ya kudhuriwa na mabondia mbali mbali nchini wakiongozwa na Japhert Kaseba, Thomas Mashali. Said Mbelwa. Shabani Kaoneka na Ibrahimu Tamba mabondia ambao wanatamba kwa sasa nchini Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments: