Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya (pili kulia) wakifunua moja wa Gari aina ya Toyota IST ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Promosheni mpya ya Yatosha Zaidi ambayo itawawezesha wateja wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kujishindia zawadi ya Gari kupitia droo maalim itakayokuwa ikichezeshwa kila siku kwa muda wa miezi miwili,wateja watakaojiunga na Airtel Yatosha wataingia moja kwa moja kwenye droo ya Promosheni hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akifafanua jambo wakati mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa Promosheni mpya ya Yatosha Zaidi ambayo itawawezesha wateja wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kujishindia zawadi ya Gari aina ya Toyota IST kupitia droo maalim itakayokuwa ikichezeshwa kila siku kwa muda wa miezi miwili,wateja watakaojiunga na Airtel Yatosha wataingia moja kwa moja kwenye droo ya Promosheni hiyo.
Waandishi wa habari wakichukua tukio.
Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya (pili kulia) wakionyesha kipeperushi cha Promosheni hiyo iliyozinduliwa rasmi leo kwenye viwanja vya Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Shangwe na nderemo zikiendelea...
Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi akiwa na Balozi wa Promosheni hiyo, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Ney wa Mitego akiwa kwenye moja ya magari hayo.
Sehemu ya Magari yatakayotolewa kwa washindi wa Promosheni ya Airtel Yatisha Zaidi
...Meneja wa Airtel Jane Matinde akishow love.
Burudani zilizotolewa wakati wa uzinduzi huo.
Airtel Tanzania leo imezindua promosheni kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema” promosheni hii ni nafasi ya peeke wa wateja wetu wanaojiunga na vifurshi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. Nia yetu kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono.
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi “Aliongeza Nyakundi
Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi. hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku
Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha. tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila siku”aliongeza Mallya
Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima
Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: