Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Lindi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Amir M. Mkalipa, wamefanya kikao cha kikanuni leo tarehe 21 feb 2018, katika ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, iliyopo Wailes, Lindi mjini.
Pamoja na kujadili hoja zingine zinazohusu uimara wa jumuiya mkoani Lindi, changamoto za Vijana na Walimu, suala la migomo ya wafanyabiashara, na kuwataka watendaji wa Serikali kutimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu ili kuongeza ufanisi wa Serikali katika kutatua kero za wananchi na kuleta maendeleo ya jamii, lakini pia kikao hicho kimeazimia:-
a} Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi imeitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuhusika na mauaji ya Albino. Ni lazima Serikali kushirikiana na wananchi wahakikishe ndugu zetu Albino wanaishi maisha yenye usalama, amani na furaha kwani ni haki yao kikatiba.
b} Pia, Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi linampongeza Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM (2010-2015) kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibiti-Mingoyo,
Pia inampongeza Mhe Rais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Lakini pia, UVCCM inampongeza na kumuunga mkono Mhe Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 27 ambapo baadhi ya wateule hao wanatoka kwenye jumuiya hiyo, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa UVCCM, na kudhihirisha kuwa jumuiya hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwa tanuru la kuoka viongozi wenye uwezo, waadilifu na wenye kuaminika katika jamii. Pia UVCCM imewapongeza ndugu Mboni Mhita na ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakatimize wajibu kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na ufanisi.
Pia, UVCCM Lindi inampongeza Kamanda wa Vijana Mkoa Mhe Bernard Membe-Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa karibu na Vijana na kuiwezesha jumuiya kutimiza majukumu yake.
C} Mwisho, UVCCM Mkoa wa Lindi inahimiza Halmashauri za wilaya kutenga asilimia 10% ya Mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya Vijana na Wanawake, ili vijana wanufaike kwa mikopo na waweze kujiajiri ili kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini. Jambo hili lipo kisheria sio ombi, hivyo watendaji husika wa Serikali wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo ama UVCCM itawalazimisha kutimiza wajibu huo.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, wamepitisha ratiba ya shughuli zao kwa Mwaka 2015 na wataanza ziara ya kutembelea Vijana katika wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Lindi.
Imetolewa na:-
SAID Y. GOHA
KATIBU WA UVCCM MKOA, LINDI.
Toa Maoni Yako:
0 comments: