Alianza kuingia shemeji yangu ambaye ni askari ila alivaa kiraia baadae akafata Mme WANGU mpenzi Franco... ambae alipofika mlangoni aliganda tu... Alishikilia mlango tu akinitazama Mimi na Kelvin... huku machozi yanamtoka... kamasi zinamwagika... akaniangalia... shemeji akanitazama akasema hapa ndiyo msibani? Kabla sijajibu kitu Shemeji alinipiga kibao kimoja kupitia Kitano cha bastola yake nikakwepa kikanichana mgongon juu ya bega. Nikakimbilia kwenye godoro.
Shemeji akamvamia Kelvin akaanza kumpiga vichwa yule Manager wa hoteli akaanzaa kuzuia huku akiniambia mama vaa tauro... wakat huo Franco amesimama tu mlangoni anatetemeka hadi unaona kabisa anatetemeka... jasho linamtoka... badae akavua sandals alizokuwa amevaaa akasimama pale pale... muda wote huo ananitazama Mimi tu.
Yule muhudumu na meneja walifanikiwa kumtuliza shemej yangu...Shem akanifata akaniita kwa jina langu Mimi (tumeliweka kwenye mabano)akaniuliza umefanya nini? Mbona familia yetu ilikuamini na kukupenda sana... imekuwaje umefanya hivi?... kilikupata nini shemej yangu. Shemeji nae anaongea kwa kulia kabisa... akasema unataka ummalize Franco ukoo wake ufe? maana kabaki peke yake... hana dada wala kaka (shemeji ni Mtoto wa babake mkubwa Franco).
Ghafla nilianza kuishiwa nguvu... kuanzia miguuni ganzi ikaaanza kupanda kuja mapajani baadae kwenye vidole na mikono.mwisho nikasikia kizunguzungu nikakosa nguvu nikalegea kabisa na kuangukia kitandani style ya ubavu kwa kulala... nasikia ... naona. Lakini sijui nilipatwa na kitu gani sikuweza kunyanyua mdomo... sikuweza kutikisa hata kidole kimoja mapigo ya moyo yalibadirika nalia machozi hayatoki kabisa yamekata ila jasho linanimwagika kama maji.
Namuona Kelvin anavaaa nguo lakini damu zinavuja puani sana baadae muhudumu namuoana anavyonifunika taulo shemeji anaongea kilugha na Franco kumsihi asiwe vile alivyo nikasikia akimwambia tamka chochote moyo upumue... usiwe hivyo utakufa? Ongea chochote maana toka ameniona pale alisimama mlangoni hakutamka neno lolote... aliendelea kulia huku machozi na makamasi yanamtiririka.
Mimi nilipo naona naoka kila kitu kinaendelea lakini siwezi fanya jambo lolote ... sina nguvu na ulimi kama umekatwa... sikuwahi kupata mshtuko wa aina hii toka nimezaliwa... ingekuwa sio fahamu kuwepo naona ningekuwa nimekufa.
Nakumbuka Franco alisogea mbele akanitazama kwa upole akaniambia sikustahili haya mke wangu... sina nilipokosea mke wangu, kustahili adhabu hii... naapia kama niliwahi kutembea nje ya ndoa toka nimekuoa... basi nife kifo cha mateso... kwanini uliamua kufanya hivi... nini kilikusibu mke wangu... akalia sana kisha akasema UTANIKUMBUKA. Akainuka akatoka shemeji akanitazama akasema wewe... bahati yako...haya endeleeni wakatoka wakatufungia mlango.
Walipoondoka Kelvin alinitazama nilikua nimechanika mdomo na jicho moja lilikuwa jekundu sana akaniambia pole... sikuweza kujibu alivaaa yeye akanivalisha nikiwa kitandani baadae akampigia simu rafiki yangu mmoja aje yeye pia aliogopa kwa hali niliyokuwa nayo' maana mie sijui nini kilibishika nikawa nimepooza.
Baadae walikuja rafiki zangu wawili wakaanza kuninyoosha kwa kunipia piga misuli kwa mbali nikahisi ufahamu ila koo lilikuwa linauma na ulimi bado haukua ukinyanyuka vizuri... wakanibeba hadi kwenye gari kwa kujikongoja nguvu zimeisha kabisaaaa tukaenda hadi kwa rafiki yangu Ilala... nguvu zikaanza kuja taratibu sana nikaweza kuongea macho yakaaanza kutoka sasa nalia kama nimefiwa nawaza narudije kwa Franco niliumia sana.
Baadae Kelvin alituacha kwenda hospitali akatibiwe majeraha baadae alipiga simu nipelekwe wakanicheki na mimi nikapelekwa wakanishona nyuzi NNE tukarudi nyumbani kwa rafiki yangu wakawa wananifariji.
Ilipita Siku mbili nikamfata shangazi yang anipeleke kwangu... ilibidi nimsimulie kila kitu kilichotokea yeye alinijibu nimewatia aibu ila alinisihi nisimwambie mama kwanza tukaenda wawili kufika tukaingia tukamkuta amelala anaangalia movie sebuleni akatupokea vizuri tu.
.........akamkaribisha shangazi akampa juice na mimi akanimiminia akanikaribisha ... nilipata faraja sana baadae akasema anataka kutoka hivyo tuseme tulichofuata... Shangazi akajieleza sana lakini Franco alianza kulia akasema shangazi niko tofauti na baadhi ya wanaume. Mimi ni mpumbavu kuliko wote ndiyo maana binti yako ameweza kunichezea hivi... mama yangu alikufa nilipozaliwa .nimekosa upendo wa mama nikaweka upendo wangu wote kwa mke wangu... nilimpa kila anachotaka mke wangu... alilibadirikia ghafla... Muongo.. msiri... Sijui alikosa nini... akashindwa kulinda upendo WANGU.
Alieleza mengi jinsi alivyokuwa akinifatilia anasema pale alielekezwa kwa njia ya simu. Alisaidiwa na best friend wake ambaye alikuwa anafanya katika mtandao wa simu (jina kapuni). Pia yule shemeji yangu alisaidia kujua niko wapi kwa system yao wanayotumia huko kazini kwao ndiyo maana walifika anasema yeye aligundua siku nyingi nachepuka na hakutaka kuambiwa alikuwa akinionya tu labda nitaacha mwisho akasema hataniacha hadi athibitishe hivyo hatanisamehe kamwe.
Alieleza sana jinsi inavyotumika kukukamata kama wakihitaji na imlicost sana. Basi alisema nikiendelea kumuona hapa nitazidi kuumia nitamfanya kitu kibaya hatasahau mtanipa kesi.. Shangazi kama mmemchoka mtoto wenu mwacheni hapa ila kama mnampenda naomba nendeni nae.
Alikataa kabisa nikamfata kwa magoti akagoma akasema ana hasira niondoke zikiisha ataniita... tukaondoka na aunt... kesho yake nikapigiwa simu na Mchungaji kanisani tulikokuwa tunaabudu niende ofisini kwake... nilienda nikiwa mpole nimevimba macho kwa kulia nikamkuta Franco nae yupo huko na yule shemeji yangu askari aliyekuja nae Mkuranga wakati wa fumanizi.
Akaeleza kwa Mchungaji kisha akasema nilimchukulia hapa... mkatubarikia hapa... namuachia hapa... tukitoka hapa atafute pa kwenda.... Kama kutakuwepo na anachodai aende mahakamani nitakutana nae huko na nitamlipa anavyodai.... Nguo zake nimeshusha kwa Mama Aggy (Ni mama anayefanya usafi kanisani na ofisi kwa Mchugaji). Akaniadai funguo za gari yake... badae akasema ah! gari nakuachia vingine atafanya Kelvin... kama tulisaidiana nae vingine basi na huduma achangie... nwambie akutafutie pa kuishi... akujengee... ukija nyumban utatoka maiti.
Mchungaji alimsihi sana Franco aliondoka bila kujibu chochote... Mchungaji akasema hana jinsi ila atazidi kuongea nae laini pia sheria za kanisani kwetu lazima nitengwe nipewe adhabu kwa dhambi ya uzinzi.
Nilirudi kwa shangazi akasema tumpigie mama simu tumueleze mama alilia sana, alinisema sana akampigia Franco aongee nae Franco alikataa akanwambia mama, too late and am sorry sihitaji maongez juu yake.
Mama alikuja toka kwake tukaenda kwa Franco... tukaambiwa kachukua likizo kaenda kupumzika South Africa... Na hiyo safari ilikuwa twende wote na yeye alikuwaga ameniambia nifanye research tufikie hoteli gani nzuri... ameenda peke yake... nikaaanza kulia.
Ulipita mwaka... mzima nikiwa na Kelvin baada ya Franco kunikataa... Mungu akaniadhibu tena Kelvin alienda kuoa UK na alioa kwa siri... nilijua baada ya ndoa yake... nilikuwa kama kichaa
Nilisikia kuna mdogo wake Franko amefariki... nikaenda msibani na rafiki zangu nikaonyeshwa msichana anayeishi na Franco kwa sasa... Franco kanisani Kahama sijui anasali wapi kifupi haeleweki maana nilijua nitamuona kanisani tu... mbaya zaid binti hugo nilikuwa namjua alikuwa jirani yetu na alikujaga... kumsidia aunt yake vikazi vya ndani baada ya kutoka kijijini nikasema poor Franco... ameenda kuchukua kasichana kadogo kiasi hiki?? Aliponiona msibani alishtuka ila hakunisemesha lolote ndugu baadhi walinipokea wengine walinichunia.
Najipa moyo iko Siku nitarudi kwa Franco wangu tu!
HIVI NDIVYO NILIVYOACHWA NA FRANCO... NATOA UJUMBE KWA WANAWAKE WENZANGU. KAMA MME WAKO ANAKUPENDA ... MUHESHIMU MIMI HAPA NIMEPOTEZA DIRA YA MAISHA YANGU... FAMILIA NZIMA IMENIDHARAU MAMA KILA AKINIONA ANANISEMA... KIWANJA CHA FRANK KIPO TU... NIMEPANGA NYUMBA YANGU NAISHI. NAKULA... LAKINI BADO SIJAKIDHI HAJA YA MOYO WANGU NAJIULIZA IKO SIKU FRANCO ATARUDI KWANGU??? MUNGU ANAJUA.
Asanteni sana, Mungu awabariki na huu ndiyo mwisho wa hadithi iliyomtokea msomaji wangu niliyoipa jina la 'USITUPE MBACHAO KWA MSALA UPITAO'.
Toa Maoni Yako:
0 comments: