Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ), Joachim Mushi (kulia) akitoa poe na kisha kukabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000/-) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM ya Njombe Bw. Conrad Mpila kama pole toka TBN baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing, Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
"Tupo nawe katika wakati huu mgumu..." anasema Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ) Bw.
Joachim Mushi wakati anakabidhi ubani huo.
Joachim Mushi wakati anakabidhi ubani huo.
"Pole sana Conrad", Bw Mushi anamfariji mfiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: