Mpumzike kwa amani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Familia ya marehemu Kapten David Mpila, waliofariki kwa kuteketea na moto ndani ya nyumba yao huko Kipunguni jijini Dar es Salaam. Makamu wa rais aliongoza maziko ya familia hiyo wakati wa mazishi yao yaliyofanyika jana Februari 10/2015 katika makaburi ya Airwing Ukonga.
Mofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima za mwisho.
Majeneza yenye miili ya watu sita wa familia moja waliofariki kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto eneo la Kipunguni ‘A’ jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Februari 7, ambao walizikwa katika makaburi ya Airwing Ukonga, Dar es Salaam leo.
 Tutawakumbuka daima...
 Askari wa JWTZ wakiwa wamebeba moja ya jeneza la marehemu waliofariki katika ajali ya moto wakati wa mazishi yao.
 Fatuma Issa ambaye ni mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali hiyo akiweka udongo katika makaburi la watoto wake.
 Mtoto pekee aliyenusurika katika ajali hiyo, Emmanuel mpila akiweka udongo katika kaburi la baba yake, Kapteni mstaafu wa JWTZ, David Mpila.
 Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka shada la maua.
 Fatuma Issa akiweka shada la maua katika makaburi ya watoto wake Celina na Pauline.
 Mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali ya moto, Fatuma Issa akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake, Celina.
 Emmanuel Mpila akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake, Pauline, Emmanuel alipoteza watoto wawili katika ajali hiyo.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiweka shada la maua.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiweka shada la maua.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya akiweka shada la maua.
 Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani akiweka shada la maua.
 Fatuma Issa mama wa watoto wawili waliofariki katika ajali ya moto akiwa amezimia.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye makaburi ya familia ya marehemu Kapten David Mpila aliyefariki kwa kuteketea na moto.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji mama mzazi wa marehemu bibi Celina Mpila mke wa marehem Kapten David Mpila waliofariki kwa kuteketea na moto, wakati wa mazishi yao yaliyofanyika jana katika makaburi ya Airwing Ukonga Dar es salaam.
 Mama mzazi wa Kapteni David Mpila akiweka udongo katika kaburi la mtoto wake marehemu David Mpila leo wakati wa mazishi ya watu sita waliokufa kwa ajali ya moto baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia Februari 7.
 Waombeleji wakielekea makaburini.

 Baadhi ya watu wakielekea makaburini.
 Wanafamilia wakiwa na huzuni baada ya miili kuwasili nyumbani. Picha zote na Francis Dande.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: