Mrembo aliyetetemesha na sikendo ya kuongeza umri na kufanikiwa kunyakua taji la Miss Tanzania 2014 na hatimaye kulibwaga, Sitti Mtemvu ameamua kurudi nchini Tanzania kimya kimya baada ya kukimbilia ughaibuni kwa kipindi kirefu na kwasasa anajiachia viwanja mbali mbali vya starehe.
Kwa mujibu wa Pita Pita za Kajunason Blog, Ziliweza kumnyaka mrembo huyo mwanzoni mwa wiki iliyopita katika kiwanja kimoja cha starehe akijivinjali na wenzake.
Bila kujua mrembo huyo aliongea na Mdodosaji wa Kajunason Blog maneno ambayo kiukweli yalionyesha ni mwenye furaha, ni baada ya wenzake kumwambia kuwa anajisikiaje kuwa huru, alijikuta akisema “Ahaa! Kwa sasa anibabaishi mtu nakula starehe kwa raha zangu, walitaka kunizeesha na maneno maneno utadhani mimi nilikuwa wa kwanza kupata skendo kama ile,”.
Sitti akishow love na wenzake.
Sitti akivinjali na marafiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: