Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo , wakati akitoa Fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Januari, 2015. Kulia ni Kaimu Meneja Idara ya Takwimu za Bei na Ajira, Hashim Njowele.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale.

MKURUGENZI  wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahimu Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi januari 2015 umeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 4.0 kutoka 4.8 Desemba mwaka jana.

Mbali na mfumuko wa bei kushuka pia thamani ya sh. ya Tanzania imeshuka mwezi Januari 2015 ikilinganishwa na Septemba 2010.

''Uwezo wa shiringi ya tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh. 65.60 mwezi Januari kutoka mwezi semptemba," alisema.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana Kwesigabo alisema kupungua kwa bei hizo kunamanisha kupugua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi  Januari.

"Mfumuko wa bei wa taifa umeendelea kupungua hadi kufikia asilimia 4.0  kwa mwezi Januari ikilinganishwa na asilimia 4.8 ilivyokuwa mwezi Desemba 2014,"alisema. 

Kwesigabo alisema bei za vyakula na vinyaji baridi zimeendelea kupungua hadi asimilia 4.9 mwezi Januari 2015 kutoka asilimia 5.7 mwezi Desemba 2014.

"Fasuli za bei zimeongezeka hadi 152.43 kwa mwezi Januari kutoka 146.60 kwa mwezi Januari 2014,''alisema. 

Aliongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujunishi bei za vyakula na nishati umeendelea kupungua kwa mwezi Januari 2015 hadi  kufikia asimilia 2.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwezi Desemba 2014.

"Mfumuko wa bei wa bidhaa umeendelea kupungua kulingana na kipimo cha mwezi Januari mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 0.1 hali ambayo inaonesha kupungua kwa mfumuko wa bei," alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: