Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiingia katika ofisi za Kampuni ya Habari Corporation Ltd, kendelea na ziara katika vyombo vya habari aliyoianza wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Godfrey Chongolo.
 Nape akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Habari Corporation Denis Msaky baada ya kuingia chumba cha habari.
 Napa kisalimiana na Mhariri wa Msanifu wa Habari wa Mtanzania Hamis Mkotya.
 Nape akiwa katika chumba cha habari cha Mtanzania.
 Nape akitazama picha iliyomvutia katika chumba cha habari cha Mtanzania, ambayo alionyeshwa na Msaky.
 Picha yenyewe ni ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Muasisi wa Habari Corporation, Jenerali Ulimwengu.
 Nape akionyeshwa chumba cha habari cha chenye mkusanyiko wa madawati mbalimbali ya magazeti ya Mtanzania Rai na Dimba.
 Nape akisalimiana na Mhariri wa habari wa Mtanzania, Bakari Kimwanga.
 Nape akisalimiana na John Mlinda.
 Nape akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Usanifu.
 Nape akiwa katika picha ya pamoja na wasanifu wa kurasa.
 Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda akimkaribisha Nape.
 Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda, akitambulisha kwa Nape uongozi wa magazeti ya kampuni hiyo.
 Nape akizungumza zaidi.
 Nape akizungumza mambo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Corporation, Hussein Bashe baada ya mazungumzo ya ndani.
 Wakuu wa New Habari Corporation wakiagana na Nape nje ya ofisi za kampuni hiyo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa na Mhariri Mkuu wa Mwananchi, Bakari Machumu baada ya kuwasili kwenye ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd leo.
 Bakari Machumu akimkaribisha Nape ofisini kwake. Kushoto ni Chongolo.
 Nape na Machumu akiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi na The Chitizen.
 Nape akizindikizwa na Machumu wakati wakienda ukumbini kwa ajili ya mazungumzo zaidi.
 Nape akizungumza na uongozi wa magazati ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.
 Nape akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd.
 Nape akimpatia zawadi ya kalenda ya CCM, Bakari Machumu, mwishoni mwa mazungumzo.
 Haya kwaherini mbaki salama...
 "Mimi pia nipo hapa" Angetile Oseah akimwambia  Nape baada ya kukutana wakati akiondoka ofisi za Mwananchi Communication Ltd.
 Nape akiagana na Bakari Machumu mwishoni mwa mazungumzo. Picha na Bashir Nkoromo.

Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Amesema, ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi gani.

"Chama hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", alisema Nape.

Alisema, kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu... huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona kama anatosha", alisema Nape.

"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: